Mashabiki wa Ivory Coast wakifurahia ushindi wao dhidi ya DRC

  • | VOA Swahili
    1,339 views
    Fainali ya Jumapili itakuwa na taswira ya marudio ya mchuano wa makundi kati ya Ivory Coast na Nigeria, wa Januari 18, ambapo Super Eagles walishinda 1-0.⁣ ⁣ Wakati huo huo, DR Congo italazimika kuwania nafasi ya tatu mjini Abidjan Jumamosi dhidi ya Afrika Kusini.⁣ ⁣ Walikuwa na matumaini ya kushinda hadi fainali ya kwanza ya Kombe la Mataifa tangu wawe mabingwa, wakati huo nchi yao ikijulikana kama Zaire, mwaka 1974, nusu karne iliyopita.⁣ ⁣ Jumatano, Nigeria walifuzu kkuingia fainali baada ya timu yao Super Eagles kuwacharaza Bafana Bafana ya Afrika Kusini, mabao manne kwa mawili, kupitia mikwaju ya penalti.⁣ ⁣ ⁣⁣⁣ #AFCON #Leopard #DRC #Afrikakusini #Soka #supereagles #fainali #mechi