Mashindano ya michezo ya shule za sekondari katika kaunti ya Nandi yakamilika

  • | Citizen TV
    229 views

    Mashindano ya michezo ya Shule za Sekondari kaunti ya Nandi yamekamilika Kwa kishindo huku shule ya upili ya Cheptil, Itigo,kosirai na Chemase wakijipatia tikiti ya kuwakilisha Kaunti hiyo kwenye mashindano ya ukanda mwa bonde la ufa. Timu ya voliboli ya valuna ambayo pia ni Mabingwa wa Afrika Mashariki ,Cheptil, walionyesha ubabe wao kwa kucharaza timu ya Lelmokwo seti 3-2. Timu ya Voliboli kwa wasichana ya AIC Kosirai iliishinda Cheptil seti 3-2 huku Timu ya wasichana ya Itigo Queens ikiiibuka Mshindi wa soka baada ya kuishinda timu ya Koitabut kwa mabao 7-0. Katika Soka ya Wavulana, timu ya Chemase iliinyuka koitabut mabao 7-0 kwenye mashindano yaliyofanyika Katika Shule za Wasichana za Aldai na St..Marks Kaptumo