Mashirika katika kaunti ya Kwale yaanzisha kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu utovu wa usalama

  • | Citizen TV
    80 views

    Mashirika matano ya vijana na akina mama katika kaunti ya Kwale yamezindua kampeni ya kuhamasisha jamii dhidi ya utovu wa usalama, amani na dhulma za kijinsia ili kuimarisha uwiano miongoni mwa jamii za dini tofauti katika kaunti hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itahusisha vingozi wa kidini, wazee wa kaya na maafisa wa usalama watakaofanya vikao na midahalo mashinani katika juhudi za kutatua visa vinavyosababisha ukosefu wa amani na dhulma za kijinsia.