Mashirika ya Kijamii yataka Rais Ruto aambatanishe msamaha na vitendo

  • | Citizen TV
    1,640 views

    Mashirika ya kijamii chini ya muungano wa Okoa Uchumi yamepuuza msamaha wa rais William Ruto kwa vijana maarufu Gen Zs vikisema kwamba hauna ukweli. Wawakilishi wa makundi hayo wakizungumza mjini Machakos, wamelaumu rais kwa kutowajibikia mauaji ya vijana 60 na wengine kutekwa nyara kwenye maandamano ya Gen Z mwezi Juni mwaka uliopita.