Mashirika yakosoa polisi kushirikiana na magenge

  • | Citizen TV
    1,008 views

    Chama cha mawakili nchini LSK sasa kinasema kina ushahidi kuwa maafisa wa polisi walishirikiana na magenge ya wahalifu waliokuwa wakiwahangaisha watu na kuvuruga maandamano ya hapo jana. Aidha, idara ya mahakama pia imekosoa matukio ya hapo jana, ambapo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya magenge kuingilia maandamano ya kudai haki kwa mwanablogu Albert Ojwang.