Masomo katika zaidi ya shule tatu Kapedo hayafanyiki

  • | Citizen TV
    Masomo katika zaidi ya shule tatu zilizoko katika eneo la Kapedo Turkana Mashariki yanaendelea kutatizika na shule hizo kufungwa kabisa kutokana na ukosefu wa usalama. Wanafunzi na walimu wa shule hizo wamehamia kwingine. Tangu mwaka elfu mbili na kumi na saba shule ya umma ya msingi ya Kapedo girls ilifungwa kabisa baada ya mlinzi na mwalimu wa shule hiyo kupigwa risasi.