Masomo ya gredi ya saba na ya nane hayajatengewa bajeti ya kutosha

  • | K24 Video
    19 views

    Hisia mseto zimeibuka baada ya kubainika kuwa huenda wanafunzi wa gredi ya nane wakakosa ufadhili kutoka kwa serikali kwa kuwa hawakuzingatiwa katika bajeti ya mwaka ujao wa kifedha. Vile vile katibu mkuu wa elimu Belio Kipsang alieleza kuwa wanafunzi takriban milioni moja wa shule za upili za kutwa wanaopata masomo ya bure, huenda wakakosa ufadhili wa serikali kufuatia upungufu wa shilingi bilioni 22.2 katika bajeti ijayo. Hata hivyo waziri wa elimu Ezekiel Machogu amewahakikishia wazazi kuwa liwe liwalo watahakikisha kuwa ufadhili unawasilishwa kama ilivyo katika sheria.