Mataifa ya Afrika yajadili mikakati ya kuimarisha usalama

  • | K24 Video
    21 views

    Miaka 19 tangu kubuniwa kwa baraza la kukabili silaha ndogo-ndogo recsa, ulanguzi wa silaha hizo bado unasalia changamoto kuu katika juhudi za kuleta amani na maendeleo barani Afrika. Akihutubia kikao cha baraza hilo jijini Nairobi, waziri wa usalama profesa kithure kindiki anasema bara la afrika lina raslimali za kutosha kuinuka kiuchumi ila ukosefu wa usalama katika mataifa mengi ni kizingiti cha maendeleo. Hili likitokana na ulanguzi wa silaha ndogondogo.