Afrika kutatizika baada ya Uingereza kukata misaada. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    7,336 views
    Miradi inayolenga kuimarisha maisha ya wanawake na watoto barani Afrika inatarajiwa kuathirika zaidi na hatua ya Uingereza kukata misaada, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo. Mwezi Februari, serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa itapunguza misaada ya kigeni kwa asilimia 40% katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, kufuatia shinikizo kutoka kwa Marekani ili kuongeza bajeti yake ya kijeshi.