'Mathe wa Ngara' atafuta agizo la kutomkamata

  • | Citizen TV
    1,161 views

    Mfanyibiashara Nancy Kigunzu maarufu kama 'Mathe Wa Ngara' ameelekea mahakamani akitaka mahakama itoe agizo la kuzuia kukamatwa kwake. Kigunzu anadai kuwa polisi wanamsaka na nia ya kumfungulia mashtaka asiyoyajua akisema kukamatwa kwake kutaathiri biashara anazofanya nchini. Kigunzu amesema yuko tayari kujisalimisha iwapo atapata kuskizwa na haki kufanyika. Kusakwa kwa kigunzu kunajiri kufuatia kukamatwa kwa washukiwa watatu wakati wa oparesheni ya polisi eneo la ngara ambapo zaidi ya shilingi milioni 12 na magunia 26 ya bhangi yalipatikana. Kesi dhidi ya watatu hao iliendelea leo katika mahakama ya jkia ambapo ilibainika wawili miongoni mwao ni watoto ambao bado hawajafikisha umri wa miaka 18