Matiangi atangaza operesheni kuu katika maeneo ya Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet na Baringo

  • | K24 Video
    135 views

    Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi ametangaza kuanzishwa kwa operesheni kali katika maeneo ya Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet na Baringo. Matiang'i amesema kuwa serikali imefanya kila iwezalo kurejesha hali ya amani ila mbinu zote ikiwemo mazungumzo na wananchi na hata viongozi zimeambulia patupu. Vile vile Matiangi amedokeza kuwa huenda kukawa na agizo la kutotoka nje ili kufanikisha operesheni hiyo.