Matokeo ya KPL

  • | Citizen TV
    255 views

    Timu ya Police Fc imepoteza mechi yake ya pili mfululizo kwenye ligi kuu nchini baada ya kulazwa moja bila na Kakamega Homeboyz uwanjani Ulinzi Complex. Walinda doria hao waliingia mchezoni baada ya kutocheza wikendi iliyopita, wakianza vyema mechi hiyo ila wakasalimu amri kwenye dakika ya 89, wakati mchezaji wa akiba Shuma Moses alipopiga bao hilo la pekee kwa wageni Homeboyz. Kwenye mechi nyengine uwanjani humo, Ulinzi Stars wameilaza Posta Rangers bao 1-0.