Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Mchakato wa kuhesabu kura baada ya kumalizika kwa upigaji kura

  • | BBC Swahili
    6,475 views
    Mamilioni ya Wakenya siku ya Jumanne walishiriki katika shughuli ya upigaji kura kuwachagua viongozi wao baada ya kampeni kali iliyotawaliwa na mijadala kuhusu gharama ya maisha, ukosefu wa ajira na ufisadi. Na katika makala hii tunaangazia jinsi kura zinavyohesabiwa baada ya wananchi kutekeleza wajibu wao wa kujitokeza na kupiga kura kulingana na maagizo na masharti ama ya Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) au Katiba. #bbcswahili #matokeoyauchaguzi2022 #kenya