Profesa David Ndetei ameifahamisha mahakama kuu ya Milimani kuwa yeye binafsi aliandika na kutia saini hati ya kiapo iliyopinga kuachiliwa kwa dhamana kwa aliyekuwa mkewe Rose Mbithe, watoto wake wawili na washukiwa wengine wanne wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Dkt. Victoria Mutiso. Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Alexander Muteti, profesa huyo mwenye umri wa miaka 77 alisisitiza kuwa yaliyomo kwenye hati hiyo ni ya kweli. Aidha, aliifahamisha mahakama kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa Mbithe na watoto wao wawili kutokana na mzozo wa ardhi katika Kaunti ya Machakos pamoja na matatizo yaliyokuwepo katika ndoa yake na Rose Mbithe.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive