- 504 viewsKesi ya kubaduliwa kwa Rigathi Gachagua Kama naibu rais inaendelea kusikizwa huku Gachagua akisisitiza kuwa mchakato wa kumbandua haukufuata sheria. Kupitia kwa mawakili wake, gachagua ameeleza jopo la majaji watatu kuwa mchakato huo haukuafikia viwango vinavyohitajika vya kikatiba na ushirikishwaji wa umma. Aidha Gachagua anaitaka mahakama kutathmini iwapo mchakato wa kumtimua ulifuata sheria kikamilifu.