Mawakili waandamana nchini wakitaka korti iheshimiwe

  • | Citizen TV
    834 views

    Chama cha Wanasheria nchini LSK kiiliandaa maandamano katika matawi yake kote nchini, huku Mwenyekiti Eric Theuri akiapa kulinda uhuru wa idara ya Mahakama, dhidi ya vitisho na kuingiliwa na rais William Ruto. Aidha, wanachama wa LSK wakiwemo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake kutoka chama cha DAP - K Eugene Wamalwa, wamekashifu Bunge kwa kuendeleza shughuli ya kukusanya maoni ya mswada wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu licha ya shughuli hiyo kusimamishwa na mahakama.