Chama cha wansheria humu nchini kimetakiwa kusimama kidete katika kupigania haki na utawala bora huku nchi hii ikielekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Akihutubia hafla ya kuweka jiwe la msingi la jumba la Wakili Towers jijini Nairobi, Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen alisema chama hicho ni nguzo muhimu ya kuhakikisha serikali inawajibika, na akawahimiza mawakili kutekeleza wajibu wao ili Kenya iweze kuheshimu utawala uliojikita kwenye sheria. Jaji Mkuu Martha Koome, aliyehudhuria hafla hiyo, alisema mradi wa jumba la Wakili Towers utaimarisha mchango wa mawakili katika mfumo wa utekelezaji haki humu nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive