Mazungumzo ya serikali na madaktari yakwamia katika utiaji saini

  • | K24 Video
    82 views

    Sekta ya afya iliyo taabani bado haijapata tiba kwani mgogoro kati ya madaktari na serikali ungali unaendelea. Muungano wa madaktari nchini, KMPDU umesusia kutia saini mkataba wa kurudi kazini. katika mkutano na kamati ya kitaifa ya kutatua mgogoro, ambao uliendelea hadi usiku wa manane, tuhuma na majibu kutoka pande zote yalisababisha kusimama kwa mazungumzo. KMPDU Inasisitiza kuwa mgomo bado unaendelea huku ikiishutumu serikali kwa kukataa kutoa muda wa kutekeleza ahadi zake na kushughulikia masuala yaliyoangaziwa katika notisi ya mgomo