Mbosso: 'Naishi maisha yangu ya kawaida licha ya kuugua maradhi ya moyo'

  • | BBC Swahili
    12,511 views
    Mwanamuziki wa kizazi kipya na mashuhuri sana nchini Tanzania Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kama @mbosso_ anasifika sana kwa muziki wake, maneno yakimtoka moyoni. Lakini Mboso anaugua maradhi ya moyo. Hivi karibuni aligunduliwa na tatizo la moyo kwa jina arteriosclerosis, ambalo husababisha uchungu kifuani na pia mikono yake hutetemeka. Ni vipi basi hali yake ya afya imeathiri maisha yake ya kila siku hususan kama msanii. Mwandishi wa BBC @saidaswaleh amekutana na msanii @mbosso_ Jijini Dar Es Salaam. 🎥: @frankmavura #tanzania #bbcswahili #sanaa