Mbunge Kaluma atishia kurejea tena mahakamani kufuatia uamuzi wa mahakama kuhusu usajili wa mashoga

  • | K24 Video
    69 views

    Kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu ya kuruhusu usajili wa vikundi vya LGBTQ mbunge wa Homabay Peter Kaluma ametangaza kuwa ataelekea mahakamani tena kuomba kuzuia marekebisho ya ibara ya 27 (4) ya katiba ambayo inafafanua jinsi ya kujumuisha maelekezo ya mazingira ya jinsia. Wakati huohuo shirika la kutetea haki za kibinadamu KHCR limepongeza mahakama hiyo kwa kuruhusu usajili wa mashirika ya jamii hiyo ya LGBTQ