Skip to main content
Skip to main content

Mbunge Ndindi Nyoro akosoa ikulu kwa gharama yao ya juu ya bajeti

  • | Citizen TV
    860 views
    Duration: 1:37
    Bajeti ya Ikulu, ambayo sasa imefikia shilingi bilioni 16.9 kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026, imeendelea kukosolewa hii ikiwa karibu mara mbili ya mgao wa awali wa shilingi bilioni 8.6. Akizungumza huko Kambirwa, Kaunti ya Murang’a, Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema serikali haiwezi kuendelea kutanguliza gharama za juu ambazo sio muhimu huku mahitaji ya msingi ya wananchi yakipuuzwa. Nyoro ameitaka serikali kuelekeza rasilimali za taifa katika maendeleo na huduma muhimu za umma akisisitiza uwajibikaji na matumizi ya busara ya fedha za walipa ushuru.