Mbunge wa Juja akabiliwa na mashtaka ya kughusi vyeti vya masomo

  • | Citizen TV
    1,203 views

    Mbunge wa Juja George Koimburi ameachiliwa kwa dhamana ya shillingi elfu 200,000 baada ya kufikishwa mahakamani kwa mashtaka kadhaa yakiwemo kughushi vyeti vya masomo. Mbunge huyo aliyekamatwa siku ya jumanne anakabiliwa na mashtaka saba lakini alijibu mashtaka sita pekee, la saba ambalo ni kukosa kufika mahakamani katika tarehe kadhaa mwaka wa 2021 likiibua vuta nikuvute kati ya upande wa mashtaka na mawakili wa Koimburi.