Skip to main content
Skip to main content

Mbunge wa Malindi Amina ataka mazungumzo chamani ODM

  • | Citizen TV
    1,133 views
    Duration: 1:15
    Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi Sasa anautaka uongozi wa chama Cha ODM kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi na wanachama wanaopinga uongozi huo ili kukabiliana na migawanyiko inayoshuhudiwa chamani humo. Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa bweni katika shule ya upili ya Jilore, Mnyazi anasema misingi ya chama hicho imekuwa kufanya mazungumzo wakati uongozi wake unapopitia changamoto. Mbunge huyo ameshikilia kuwa licha ya mgogoro huo, wafuasi wa pande zote wanasistiza kusalia wanachama wa chama cha chungwa.