Mbunge wa Mwingi Magharibi Charles Nguna atetea hazina ya CDF

  • | Citizen TV
    466 views

    Mbunge wa Mwingi magharibi Charles Nguna amemrai rais William Ruto kuokoa hazina ya ustawishaji wa maeneobunge CDF iliyobatilishwa na mahakama. Kulingana naye, hazina hiyo imewasaidia wanafunzi wengi nchini kutoka familia masikini ambao hawangemudu gharama ya elimu. Mbunge huyo anaonya kwamba wakenya wengi waliotegemea hazina hiyo watateseka sana iwapo haitarejeshwa