Mbunge wa Ugenya alaumiwa kwa kuunga mkono serikali

  • | K24 Video
    259 views

    Kulitokea kizaa-zaa hii leo katika eneo bunge la Ugenya kaunti ya Siaya kilichowaacha watu kadhaa wakiwa na majeraha baada ya wafuasi wa ODM kukabiliana na wafuasi wa mbunge wa eneo hilo David Ochieng mbele ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga. Wafuasi wa ODM walimkemea ochieng kwa kuegemea upande wa serikali huku viongozi wengi wakilaumu utawala wa rais William Ruto kwa kutotimiza ahadi za kampeini yake.