Mbuzi 50 kati ya 380 walioibiwa warudishwa Maralal

  • | Citizen TV
    411 views

    Kikosi cha usalama kimekuwa kikifanya operesheni ya kurejesha mbuzi walioibwa katika kijiji cha Loikas, mjini Maralal. Hamsini kati ya mbuzi 308 walioibwa mwezi jana wamepatikana. Wafugaji eneo hilo wanaitaka serikali kuimarisha usalama ili kuzuia visa vya wizi wa mifugo kwani vinawasababishia hasara kubwa. Oparesheni hiyo inaongozwa na Naibu Kamishna wa Kaunti ya Samburu Titus Omanyi. Polisi wanasema kuwa wanazidi kufuatilia kisa hicho ili kuwarejesha mifugo wote walioibiwa.