Mchezo wa Skate unavyowasaidia watoto wa mitaani kuponya majeraha

  • | BBC Swahili
    327 views
    Eric Cyubahiro, aliyewahi kutumikishwa jeshini akiwa mtoto amekuwa akisaidia zaidi ya watoto 200 kuondoka mitaani katika miji kadhaa nchini Rwanda kwa ikiwa ni pamoja na kuwaingiza katika mchezo wa Skate ambao unazidi kuwa maarufu nchini humo. Aliwarudisha shuleni na kuwasaidia kupata sare za shule na chakula na sasa maisha yao yamebadilika. Anasema anatumia mchezo huo kama tiba ya kuponya majeraha yasiyoonekana ya watoto wa mitaani. #bbcswahili #rwanda #skate Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw