Mchuuzi aliyepigwa risasi na polisi ameaga dunia

  • | Citizen TV
    8,727 views

    Mchuuzi aliyepigwa risasi na polisi katikati ya jijini la Nairobi Boniface Mwangi Kariuki ameaga dunia. Kijana huyu wa miaka 22 amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya kenyatta kwa takriban majuma mawili. Madaktari hapo jana walikuwa wameiambia familia kuwa ubongo wa Kariuki ulikuwa haufanyi kazi kabisa.