Mchuuzi wa barakoa aliyepigwa risasi na polisi Nairobi aaga dunia

  • | KBC Video
    26 views

    Boniface Mwangi Kariuki ambaye ni mchuuzi wa barakoa mwenye umri wa miaka-22 aliyepigwa risasi mnamo tarehe 17 mwezi huu wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Nairob, ameaga dunia. Kulingana na Jonah Kariuki Nyambura, mwanawe wa kiume alifariki mapema leo mwendo wa saa tisa na dakika kumi na tano alasiri. Marehemu alikuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta tangu tarehe 17 mwezi huu, baada ya kupigwa risasi jijini Nairobi. Wakati wa kulazwa kwake hospitalini humo, gharama ya matibabu ya Kariuki ilikuwa imefikia shilingi milioni-3.6 ,fedha ambazo familia hiyo imesema haiwezi kumudu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive