Baraza la Vyombo vya Habari Nchini (MCK) limewasuta baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kukosa kuwalipa wanahabari. Akizungumza katika Kaunti ya Nakuru, Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, David Omwoyo, amekashifu vyombo vya habari kwa kutowajali wanahabari na mazingira wanayofanyia kazi. Omwoyo amesema kuwa, huku taifa likijiandaa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Wanahabari Jumapili, changamoto za malipo duni, kufungwa kwa ofisi za mikoani na mazingira duni ya kazi zinahatarisha uhuru wa vyombo vya habari na kuathiri ubora wa taarifa kwa umma.