Mdhibiti wa bajeti aeleza kiini cha gharama kubwa ya mishahara

  • | Citizen TV
    386 views

    Mdhibiti wa bajeti ya kitaifa Margaret Nyakang'o ameeleza baadhi ya sababu zinazoongeza mgizo wa mishahara ya watumishi wa umma nchini na kuathiri miradi ya maendeleo. Akizungumza kwenye kongamano la kitaifa kuhusu mishahara hapa Nairobi, Nyakang'o ametaja marupuru mengi, wafanyakazi hewa na malipo kwa watu wasiokuwa na manufaa kikazi kama baadhi ya malipo yanayoongeza gharama ya misharaha kwenye kaunti.