Meli iliyowabeba watalii mia nane yatia nanga katika bandari ya Mombasa

  • | KTN News
    6,349 views

    Bandari ya mombasa imeanza kushuhudia shughuli nyingi baada ya meli iliyowabeba watalii mia nane kutia nanga. Meli hiyo kwa jina Ms World Odyssey iliwasili bandarini mapema hivi leo kutoka bandari ya aqaba nchini Jordan. Waziri wa Utalii Peninah Malonza alikuwepo kuipokea meli hiyo.