Mfalme wa Uingereza aanza ziara yake ya siku nne Kenya

  • | VOA Swahili
    209 views
    - - - - - #VOASwahili Mfalme wa Uingereza Charles wa tatu anaanza ziara yake ya siku nne nchini Kenya Jumanne ikiwa ni safari yake ya kwanza barani Afrika tangu awe mfalme kufuatia kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth mwaka jana. Malengo yake ni pamoja na kushughulikia kile maafisa wa Kasri ya Buckingham wanaeleza kama mambo yenye uchungu yaliyojitokeza wakati wa ukoloni na taifa hilo la Afrika Mashariki. Pia atajadili maswala yanayohusiana na shida ya hali ya hewa na umuhimu wa usalama wa kitaifa.