Skip to main content
Skip to main content

Mfanyabiashara apeleka chakula cha msaada Takaba, Banisa na Elwak

  • | Citizen TV
    128 views
    Duration: 1:19
    Familia zaidi ya elfu tano kutoka maeneo ya Takaba, Banisa na Elwak, Kaunti ya Mandera, zina sababu ya kutabasamu wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan baada ya mfanyabiashara kutoka Nairobi kutoa msaada wa chakula na maji kufuatia hali mbaya ya ukame inayoendelea kushuhudiwa eneo hilo. Mfanyabiasha huyo Haji Samow ametaka serikali ya kitaifa kuongeza juhudi za kuwafikia wakazi wa maeneo yaliyoathirika zaidi na ukame kwa kuwapatia msaada wa dharura, akisisitiza kuwa hali inaendelea kuwa mbaya na inahitaji hatua za haraka ili kuokoa maisha na mifugo ya wenyeji.