Mfanyakazi adaiwa kumuua mwajiri wake wa miaka 78

  • | Citizen TV
    873 views

    Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa mauaji ya mwanamke wa miaka 78 katika mtaa wa Nyathaini eneo la Kasarani hapa Nairobi. Mshukiwa Victor Ambeyi anadaiwa kumpiga mama huyo aliyekuwa muajiri wake, kumuua na kisha kuuficha mwili wake kwenye shimo la maji taka lililo ndani ya boma hilo.