- 251 viewsDuration: 53sMfanyakazi mmoja wa serikali ya kaunti ya Kilifi anakabiliwa na kesi tano za tuhuma za ulaghai wa zaidi ya shilingi milioni 5 katika matukio tofauti. Emmanuel Kithi, mfanyakazi msaidizi katika idara ya jinsia kaunti ya Kilifi anadaiwa kulaghai watu katika matukio mbali mbali akiahidi kuwapa zabuni kati ya mwaka wa 2021 hadi mwaka jana. Tayari kaunti ya Kilifi imemsimamisha kazi mshukiwa huyo ili kutoa nafasi ya uchunguzi na kusikilizwa kwa kesi zinazomkabili.