Ni mvutano kuhusu usimamizi wa mojawapo ya hospitali bora zaidi eneo la Afrika Mashariki. Hospitali ya Nairobi Hospital, inakabiliwa na mzozo wa uongozi mbali na madai ya ufisadi ambayo sasa yameingiliwa na ikulu. Na huku Rais William Ruto akiapa kuilinda Hospitali hiyo dhidi ya wale aliowataja kama matapeli na walaghai, wataalamu wa sheria wanaibua wasiwasi. Swali ni Je, Rais, katika nafasi yake kama mlezi wa hospitali ya Nairobi Hospital, ana mamlaka ya kuingilia kati maswala yaliyoibuka? Brenda Wanga anatuarifu zaidi.