- 440 viewsDuration: 1:46Rais William Ruto amesema kwamba aliamuru kukamatwa na kuondolewa mamlakani kwa watu wanne wanaohusishwa na usimamizi wa hospitali ya Nairobi hospital na ambao waliofikishwa mahakamani na kukana mashtaka ya ufisadi dhidi yao. Akihutubia umati katika eneo la mlima Elgon, rais Ruto amesisitiza kwamba kamwe hatakubali wale anaodai kuwa 'wafisadi' kuongoza Nairobi hospital ambayo inatambulika kwa sifa yake ya kutoa huduma za hali ya juu za matibabu kwa umma.