Mgombea mwenza wa Raila Odinga akutana na walimu Kiambu

  • | Citizen TV
    4,582 views

    Baadhi ya walimu kote nnchini wamekata kauli ya kuunga mkono azma ya Raila Odinga kumrithi rais Uhuru Kenyatta. Viongozi wa vyama vya walimu nchini kuppet na KNUT walikutana na mgombea mwenza wa Raila Odinga kwenye muungano wa Azimio One Kenya Martha Karua na kumpa hakikisho hilo. Karua akiahidi kwamba iwapo azimio itaunda serikali ijayo basi walimu na wahudumu wa afya ambao wamehitimu na hawana kazi wote wataajiriwa ili kuimarisha hali ya afya na elimu katika taasisi za umma nchini.