Aliyekuwa Jaji Mkuu na anayewania urais kupitia chama cha United Green Movement, David Maraga, amewahimiza vijana kujisajili kuwa wapiga kura ili waweze kutumia haki yao ya kidemokrasia katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2027 kuchagua viongozi.
Akizungumza katika mji wa Murang’a wakati wa ziara ya kukutana na wananchi inayojulikana kama Ukatiba Caravan, Maraga amekosoa vikali kile alichokitaja kuwa ufisadi uliokithiri nchini, akisema njia pekee ya kukomesha hali hiyo ni kwa wananchi, hasa vijana, kujisajili kuwa wapiga kura na kuchagua viongozi bora watakaosimamia rasilimali za taifa kwa uwajibikaji.