Mgombeaaji ugavana Nairobi Johnson Sakaja yuko huru kuwania wadhifa huo mnamo Agosti tisa

  • | K24 Video
    178 views

    Mgombea wa ugavana wa Nairobi Johnson Sakaja sasa yuko huru kuwania wadhifa huo katika uchuguzi wa Agosti tisa. Hii ni baada ya jopo la kutatua migogoro la IEBC kuondoa kesi dhidi yake. Sakaja alidaiwa kutumia shahada gushi ya chuo cha Team cha Uganda ili kuidhinishwa na IEBC. IEBC imesema sakaja aliidhinishwa kisheria na kuwa jopo la IEBC halina uwezo wa kuchunguza kashfa hiyo kisheria. Kesi kuhusu shahada gushi dhidi ya Wavinya Ndeti anayewania ugavana kaunti ya Machakos pia imetupiliwa mbali.