- 26 viewsDuration: 3:50Mafunzo katika vyuo vikuu vya umma yamekwama baada ya wahadhiri na wafanya kazi kutekeleza tisho lao la kugoma. Wafanyakazi wa vyuo hivyo vikuu waliandamana barabarani wakitaka kutolewa kwa shilingi bilioni 2.73 chini ya awamu ya pili ya makubaliano ya pamoja ya mwaka 2021–2025 ya nyongeza ya mishahara na marupurupu na shilingi bilioni 7.9 za makubaliano ya pamoja ya mwaka 2017–2021. Wanaishutumu serikali kwa kutoa ahadi isizokuwa na nia ya kutimiza licha ya kutoa shilingi bilioni 2.5, huku wakisisitiza watarejea kazini tu iwapo malimbikizi hayo yote yatalipwa. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive