- 1,546 viewsShughuli za usafiri mjini Kapsabet leo zilitatizika pakubwa baada ya mgomo wa kitaifa uliochochewa na kupanda kwa bei ya mafuta kuanza na kusababisha hali ya taharuki. Wakazi waliowajumuisha waendeshaji matatu, madereva wa bodaboda, madereva wa teksi pamoja na wasafiri walifunga sehemu ya barabara ya Kapsabet–Chavakali wakitaka serikali kupunguza gharama ya mafuta, wakisema ongezeko hilo limeathiri pakubwa shughuli za usafiri na maisha ya kila siku.