Mhubiri na mkwewe wamtendea unyama ajuza huku wakidai ni miujiza katika eneo la Embakasi Mashariki

  • | Citizen TV
    8,473 views

    Mhubiri mmoja na mkwewe katika mtaa wa Mukuru kwa Jenga eneo bunge la Embakasi Mashariki wanazuiliwa na polisi baada ya kudaiwa kumfanyia matendo ya ajabu ajuza wa miaka 61 wakisema kuwa walikuwa wakimponya. Mama huyo aliokolewa na wakazi na kukimbizwa katika hospitali ya Mama Lucy baada ya kufuja damu nyingi.