Miaka 15 ya Katiba | Rais ataka haki za kimsingi za katiba kuheshimiwa

  • | Citizen TV
    596 views

    Kenya leo imeadhimisha siku ya kwanza ya sikukuu ya Katiba huku Rais William Ruto akiendelea kusisitiza haja ya kumaliza ufisadi ili kuafikia malengo ya katiba. Rais aliyeongoza siku hii katika jumba la KICC hapa Nairobi akisema ni lazima kila idara na kila mkenya kushirikiana katika kukabiliana na zimwi la ufisadi. Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga akisema ni wakati wa muafaka wa kuifanyia katiba ya sasa marekebisho ili kuiboresha