Michael Karanga wa klabu ya Kiambu ashinda taji la Amateur Stroke

  • | Citizen TV
    381 views

    Mchezaji wa klabu ya gofu ya Kiambu Michael Karanga ndiye bingwa wa mchuano wa amateur stroke mwaka huu uliokamilika leo katika uwanja wa Karen hapa jijini Nairobi. Akiandikisha ushindi wake wa kumi msimu huu, Karanga alimaliza mchezo kabla ya mipigo 11 kuibuka bingwa mbele ya Malik Taimur aliyekuwa amesalia na mipigo mitano. Karanga ambaye analenga kuvunja rekodi ya kitaifa atakosa mzunguko ujao wa Kisumu akitarajiwa kusafiri nchini Misri kwa mchuano wa chipukizi wiki mbili zijazo.