Mifugo wauawa kwenye makabiliano ya polisi na majangili

  • | KBC Video
    109 views

    Wafugaji kutoka sehemu ya Ndumuru, Igembe kaskazini kaunti ya Meru wanakadiria hasara baada ya mifugo wao kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya wezi wa mifugo na maafisa wa polisi wa akiba. Wakati wa makabiliano hayo, ngombe saba na mbuzi watatu waliuawa huku ngombe wengine kumi na moja wakijeruhiwa. Mchungaji mmoja wa mifugo alijeruhiwa kwenye mkono wake wa kushoto.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive