| MIFUKO YA DHIKI | Wanafunzi wa shule wahusika na uchuuzi kaunti ya Kisii

  • | Citizen TV
    1,315 views

    Hebu fikiri haya, Mwanafunzi anayelazimika kutafutia familia yake riziki kabla ya kwenda kutafuta elimu. Hii ni hali ambayo inashuhudiwa katika baadhi ya shule za kaunti ya Kisii ambako wanafunzi wamegeuka wachuuzi kutokana na hali ya umaskini nyumbani kwao. Katika shule ya Daraja Mbili, hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na kuwa soko hilo limepakana na shule, na shule yenyewe haina ua. Chrispine Otieno alifuatilia maisha ya baadhi ya wanafunzi waliolazimika kufanya uchuuzi wa mifuko kila siku ya Jumatatu na Alhamisi, Kwenye Makala maalum ya 'MIFUKO YA DHIKI.'