Miili miwili zaidi yaopolewa Tana River kufuatia mkasa wa boti

  • | Citizen TV
    1,968 views

    Huku watu 23 wakisakwa, Manusura waliokuwa ndani ya boti iliyozama jana jioni mto Tana na ambao wanapokea matibabu katika hospitali moja mjini Madogo wamelaumu wasimamizi wa boti hiyo kwa kubeba abiria wengi kupita kiasi. Kwa mujibu wa polisi eneo la Madogo, Kufikia sasa ni watu 20 pekee ambao wameokolewa. Shughuli za kutafuta miili ya wanaoshukiwa kuangamia kwenye mkasa huo zinatarajiwa kuendelea hii leo baada ya kusitishwa jana usiku kutokana na giza.Naibu Gavana wa kaunti hiyo Mahat Ali Loka amesema maafisa wa kaunti hiyo wataanza kusafirisha watu kwa kutumia boti za kaunti ili kukomesha tamaa za wahudumu wa boti zinazowafanya kubeba abiria wengi na kwenda kasi.