Miili ya watu 19 waliofariki kwenye ajali ya ndege nchini Tanzania imesafirishwa kutoka Bukoba

  • | Citizen TV
    566 views

    Miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision air hapo jana imesafirishwa kutoka uwanja wa kaitaba mjini Bukoba. Shughuli ya kutoa buriani iliongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.Rais Suluhu ametuma rambirambi zake kwa familia huku uchunguzi wa kina ukianzishwa.Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amemzawadi shilingi milioni moja za tanzania kijana Majaliwa Jackson ambaye aliwaokoa watu 24 kati ya 26 walionusurika.Kijana huyo pia atapokea mafunzo ya uokoaji kutoka serikali ya Tanzania. Ndege hiyo iliyopata ajali hapo jana asubuhi ilipokuwa ikitua katika uwanja wa bukoba.